• Life Skills Discussions

  Add comments and win points

  Join, Discuss, Learn, Share idea with others

  Back to discussions

  Posted 2 years ago

         ELIMU YA SAIKOLOJIA NA KUJITAMBUA

                                                     MAKUNDI YA TABIA KUU NNE (4) ZA BINADAMU

   

   

  Habari wapendwa wote wa Shule direct!

   

  Natumaini wote mnaendelea vizuri pia tumshukuru Mungu kwa kuendelea kutulinda na kutupatia uhai.

   

   

  Leo ninapenda kuwashirikisha sehemu ndogo ya kitabu cha saikolojia ambacho ni miongoni mwa vitabu nilivyosoma ktk likizo hii ya Corona. Kitabu kinaitwa MABADILIKO YA DHATI NA KUJITAMBUA (Transformation and self-awareness) kimeandikwa na Magreth Lazaro, sitategemea kitabu hicho tu ktk kuandika mada hii ila pia nitatumia uelewa wangu kutoka kwenye vitabu mbali mbali nilivyo soma vinavyo zungumzia juu ya tabia za binanamu. 

  Nitaandika namna makundi haya manne ya watu na namna ambayo tabia zinavyoweza kuathiri maisha ya mtu binafsi na jamii kwa ujumla ingawa ukubwa au udogo wa athari za tabia za mtu hutegemea na mazingira ya mtu husika, kabla hatuja yaangalia haya makundi manne tuangalie jinsi wataalamu wa saikolojia walivyo yagawa makundi haya manne ktk mgawanyo wa makundi makuu mawili ya kisaikolojia yanayoelezea tabia mbali mbali tulizonazo na ktk hayo makundi mawili ndani yake kuna makundi mawilimawili kila moja ambayo tabia zao hulandana, makundi hayo mama ya tabia ni; Introvert na Extrovert.

   

  I) Extrovert

   

  => Extrovert ni aina ya watu ambao hawana haya (aibu), ni wachangamfu na wanamarafiki wengi pia hawana utaratibu na wapo rough sana ni wachafu kwa asili. kimsingi waweza sema ni watu wenye hisia za nje . Katika kundi hili la Extrovert kuna makundi mawili ndani yake ambayo ni Sanguine na Choleric.

   

  Tabia chache za pamoja za kundi la Introvert

   

  • Hawa hawana haya (aibu) kama introvert
  • Wapo social sana ni wachangamfu tofauti na introvert ( hawa ni wapiga makelele wazuri darasani)
  • Kiakili wapo wastani, sanasana hawapendi kufikiria I mean wavivu kufikiri!

  II) Introvert

   

  => Introvert ni aina ya watu ambao wapo na haya (aibu), hupenda kukaa pekee na ni watu wenye utaratibu n.k kimsingi waweza sema ni watu wenye hisia za ndani. Katika kundi hili la introvert kuna makundi mawili ndani yake ambayo ni Phlegmatic na Melancholic.

   

  Tabia chache za pamoja za kundi la Introvert

   

  • Ni watu wapole na wataratibu.
  • Mara nyingi huwa si waongeaji mpk wakuzoee vilivyo.
  • Ni watu ambao hawapo social,hawapendi kujichanganya na watu kwani wanaaibu sana!.
  • Hupenda mambo ya kutafakarisha sana kwasababu wana upeo mzuri wa kufikiri, mfn. Kusoma vitabu na kufuatilia hoja mbalimbali.
  1. TABIA YA SANGUINE

  Sifa zake:

   

  Ni mtu mcheshi na muongeaji sana, amejaa tabasamu, ni mtu mwenye huruma sana na mkarimu, ni rahisi kwake kufanya urafiki na mtu yeyote na anamarafiki wengi, ni mbunifu, ni mfanya biashara mzuri pia anaweza kuwa daktari mzuri, anapenda kwa moyo, anamawazo mazuri, anapenda raha sana.

   

  Udhaifu wa Sanguine:

   

  Ni mropokaji sana, si mtunza siri, urafiki wake ni pale ulipo naye tu akiondoka sehemu nyinge anasahau, anaishi utoto kila siku, si kiongozi au mtawala mzuri, ni rahisi kwake kupoteza umaarufu wake, anasahau uwajibu wake, anaishi kwa hisia, ni mtu wa kuudhi au kusababisha makwazo kwa wengine, ni mlevi, hana uvumilivu, ni mtu ayeweza kutoa maamuzi mabaya kutokatana na kutojipa muda wa kufikiri.

   

   

  2. TABIA YA CHOLERIC

   

  Sifa zake:

   

  Ni mtu mwenye maneno kiasi, ni kiongozi wa kuzaliwa, ni mtu wakupenda kufanya kazi, si mtu wa kukata tama upesi na mara nyingi hupata mafanikio chanya kwasababu ya tabia hii, si mtu wa kutishwa kirahisi na daima husonga mbele, hapendi kuonewa, anapo ona jambo lina haribika hukemea mara moja hangoji mpaka mkutano ama kikao, ni mtu wa kujiamini, ni mshindani mzuri, ni mtu wa kujaribu, hakati tama mapema, ni mtu anayependa kutegemea maamuzi yake mwenyewe.

   

  Udhaifu wa choleric:

   

  Ni mtu mwenye hasira sana, ni mtu rough, ni mkali, ni mkorofi, hana shukrani, hawezi kuomba msamaha anapofanya kosa, hujiona yupo sahihi muda wote wakati sivyo,ni mbishi, si mtu wa kumaliza kazi, hajari wengine, hajari anacho ongea, ni mgumu kubadilika, anataka kuheshimiwa muda wote, ni mtu wa kuamrisha wengine.

   

   

  3. TABIA YA MELANCHOLY

   

  Sifa zake:

   

  Ni mtu mkimya , hana maneno mengi, ni mchanganuzi, ni mtu wa vipawa vingi vya akili, ni mgunduzi (mfumbuzi wa vitu), ni mtu msafi na anaye jipenda, si mtu wa kusema ovyo au kutenda ovyo, hutumia akili kutatua mambo yanayo mkabili, ni mtu mwaminifu, si mtu wa kutoa siri ovyo, ana mapendo makamilifu kwa watu, ana uwezo sana wa kujizuia ktk kufanya mambo na siyo mwepesi wa kukata tamaa, ni mtu wa kujitolea, ni mbunifu na anajua mambo mengi sana, ni daktari mzuri sana.

   

  Udhaifu wake:

   

  Hana marafiki wengi, anachagua marafiki anao wapenda tu, anatunza hasira, ni mkimya sana, akiwa ana shida hazitoi kiurahisi hivyo ni rahisi kwake kuumizwa ndani kwa ndani, ni mtu anaye kosa amani pale anapofanya kosa Fulani kwa mwingine.

   

   

  4. TABIA YA PHILEGMATIC

   

  Sifa zake:

   

  Ni mtu mpole na mtaratibu sana, sio mwepesi wa kuonyesha hasira, anaweza kukasirika lakini asionyeshe kama amekasirika, ni mtiifu wa asili, ni mtu mchekeshaji, anapendwa kuwekwa kuwa kiongozi ingawa yeye hapiganii uongozi, anaweza kujipanga, mwema, ana mapendo ya dhati, anamarafiki wengi.

   

  Udhaifu wake:

   

  Ni mwoga sana, si mwepesi wa kuamua jambo haraka, ni mzembe wa asili, ni msahaulifu, ni mvivu wa kazi, ana aibu sana, ni mtu wa kuonewa sana, ni mtu anayefanya kazi zake taratibu sana.

  Show more
    3       25

  Comments  

  Christian Leonard   Posted on 2 years ago

  Hahaaaa! mtu atakaye patia kuniambia nipo group gani la tabia kuna zawadi yake isipokuwa Vibwengo wangu wao hawataruhusiwa kusema chochote.

  Jessica Kiliba   Posted on 2 years ago

  Mmmmmmmmhhh huo tena mtihani wa University ambao ni km aanecta kwao unaitwa University Examination tena hyoooooooooooo

  Janet Mushi   Posted on 2 years ago

  Kwa kuwa vibwengo wananjua papa wao vizuri

  Janet Mushi   Posted on 2 years ago

  Ila bana asante kwakuwa kunakitu hapo umeanza nacho ndo nilikuwa sikijui lakini haiba nilisha zisomaga

  Christian Leonard   Posted on 2 years ago

  Janet Jazia jazia basi nyama kwa vile unavyovifahamu ili watu waendelee kufaidika.

  Christian Leonard   Posted on 2 years ago

  Hahaaa! Hamna Jessica unaweza kumfahamu mtu kwa kuoanisha tabia alizo nazo na miongoni mwa tabia za kundi moja moja ila japo ni ngumu kwa mtu usie ishi naye kwa mfano watu wengi wanaweza kuniweka kwenye makundi ambayo siyo yangu kwa kuangalia vituko vyangu vya humu ila kuna watu wachache niliopiga nao story km wakifanya baadhi ya connection wanalifahamu kundi langu ambalo wengi ni vigumu kulifahamu na hata mtu akitajiwa anaweza asiamini cz tabia zangu za kwenye key board ni tofauti kbs na za uhalisia ila kuna watu wachache wanazifahamu baadhi ya tabia zangu tena miongoni mwao yupo aliyewahi kuniorodheshea mpk nikamshangaa sikuamini kbs 90% alikuwa correct.

  Glory Masikangabo   Posted on 2 years ago

  hi kwakweli big up bro chris

  CAPTAIN DE ^^^@CAPTION   Posted on 2 years ago

  kwanini huwaruhusu kusema

  Najaat Hassan   Posted on 2 years ago

  Group la machiziii

  Keisha Kira   Posted on 2 years ago

  mhhhhh acha nisikuanike ww chriss

  Keisha Kira   Posted on 2 years ago

  na next time jaribu uandike kwa lugha ya kiingereza pliiz kwa sababu kiswahili kigumu kuelewa

  Nectarios Lionheart   Posted on 2 years ago

  Extrovert group na sijakosea

  Jessica Kiliba   Posted on 2 years ago

  Heeeee yaan Necta naona unamchokoza Chriss ngoja arudi online hayo maelezo yake utaomba pooo utashushiwa essay ya ajabu hujawahi kuiona DUNIANIII

  Jessica Kiliba   Posted on 2 years ago

  Heeeee yaan na ww Najaaat ndo kbsaaa unatafuta matusi na matatizo mengine ngojeni mwnyw arudi online mtamwelezaa kwa undani zaidi

  Jessica Kiliba   Posted on 2 years ago

  Heeee na ww Teddy yaan mdogo wangu mbishi ww umeambiwa hamruhusiwi kusema unang'ang'ania mwnyw ngoja when he comes baack

  Christian Leonard   Posted on 2 years ago

  Hamna kaka Nectarios sipo kwenye kundi la Extrovert ila wengi wangedhani hivyo na kuniweka miongoni mwa kundi la tabia linalo patikana ndani ya Extrovert

  Christian Leonard   Posted on 2 years ago

  Hahaaaaaa! Najaat ndio kundi lipi hilo kama unapatia patia kdg

  Christian Leonard   Posted on 2 years ago

  Hahaaa! Keisha your free my best, hapo ndio kusaidiana ulishawahi kusikia kitu kinachoitwa Johari window?

  Jessica Kiliba   Posted on 2 years ago

  Sasa mimi mpk nije nijue tabia yako mmhhh!!!!labda na Yesu asharudi mara ya pili duniani maana sitaweza kuijua kwa urahisi

  Christian Leonard   Posted on 2 years ago

  Hahaaa! Jessica kuna mtu umemtaja n mbishi naomba uangalie kundi la watu wabishi ni kundi gan vilee, Hahaaa! Sijasema neno hapo mm simoooooo..........

  Alvin Shirima Alvin Shirima   Posted on 2 years ago

  Hii

  Ciara Jol   Posted on 2 years ago

  extrovert aina ipi hapo ndo ballaa

  Sharifa Shabani   Posted on 2 years ago

  unajua majbu yake so unaweza kujijibu mwenyewe

  Henry Danger   Posted on 2 years ago

  huna jipya

  Moureen Gasper   Posted on 2 years ago

  Philegmatic

  Ask
  Ticha
  Kidevu

  Pick a Class and Continue

  Cancel

  X
  Feedback

  We Love to Hear from You

   

   

   


  X

  Connect to your school online

  X

  Find your registered child

  Or Register a New Child Here