Gooooooooooooooood

Hey guys..is this how you welcome new friends ... I mean I joined you 5 days ago and imagine I still do not have a friend .this makes me feel dumb....anyone interested in being my friend.am kind 0f lonely when am in shule direct
word
Your so beauty
I love you nick m i wish 1 day to see you
ELIMU YA SAIKOLOJIA NA KUJITAMBUA
MAKUNDI YA TABIA KUU NNE (4) ZA BINADAMU
Habari wapendwa wote wa Shule direct!
Natumaini wote mnaendelea vizuri pia tumshukuru Mungu kwa kuendelea kutulinda na kutupatia uhai.
Leo ninapenda kuwashirikisha sehemu ndogo ya kitabu cha saikolojia ambacho ni miongoni mwa vitabu nilivyosoma ktk likizo hii ya Corona. Kitabu kinaitwa MABADILIKO YA DHATI NA KUJITAMBUA (Transformation and self-awareness) kimeandikwa na Magreth Lazaro, sitategemea kitabu hicho tu ktk kuandika mada hii ila pia nitatumia uelewa wangu kutoka kwenye vitabu mbali mbali nilivyo soma vinavyo zungumzia juu ya tabia za binanamu.
Nitaandika namna makundi haya manne ya watu na namna ambayo tabia zinavyoweza kuathiri maisha ya mtu binafsi na jamii kwa ujumla ingawa ukubwa au udogo wa athari za tabia za mtu hutegemea na mazingira ya mtu husika, kabla hatuja yaangalia haya makundi manne tuangalie jinsi wataalamu wa saikolojia walivyo yagawa makundi haya manne ktk mgawanyo wa makundi makuu mawili ya kisaikolojia yanayoelezea tabia mbali mbali tulizonazo na ktk hayo makundi mawili ndani yake kuna makundi mawilimawili kila moja ambayo tabia zao hulandana, makundi hayo mama ya tabia ni; Introvert na Extrovert.
I) Extrovert
=> Extrovert ni aina ya watu ambao hawana haya (aibu), ni wachangamfu na wanamarafiki wengi pia hawana utaratibu na wapo rough sana ni wachafu kwa asili. kimsingi waweza sema ni watu wenye hisia za nje . Katika kundi hili la Extrovert kuna makundi mawili ndani yake ambayo ni Sanguine na Choleric.
Tabia chache za pamoja za kundi la Introvert
II) Introvert
=> Introvert ni aina ya watu ambao wapo na haya (aibu), hupenda kukaa pekee na ni watu wenye utaratibu n.k kimsingi waweza sema ni watu wenye hisia za ndani. Katika kundi hili la introvert kuna makundi mawili ndani yake ambayo ni Phlegmatic na Melancholic.
Tabia chache za pamoja za kundi la Introvert
Sifa zake:
Ni mtu mcheshi na muongeaji sana, amejaa tabasamu, ni mtu mwenye huruma sana na mkarimu, ni rahisi kwake kufanya urafiki na mtu yeyote na anamarafiki wengi, ni mbunifu, ni mfanya biashara mzuri pia anaweza kuwa daktari mzuri, anapenda kwa moyo, anamawazo mazuri, anapenda raha sana.
Udhaifu wa Sanguine:
Ni mropokaji sana, si mtunza siri, urafiki wake ni pale ulipo naye tu akiondoka sehemu nyinge anasahau, anaishi utoto kila siku, si kiongozi au mtawala mzuri, ni rahisi kwake kupoteza umaarufu wake, anasahau uwajibu wake, anaishi kwa hisia, ni mtu wa kuudhi au kusababisha makwazo kwa wengine, ni mlevi, hana uvumilivu, ni mtu ayeweza kutoa maamuzi mabaya kutokatana na kutojipa muda wa kufikiri.
2. TABIA YA CHOLERIC
Sifa zake:
Ni mtu mwenye maneno kiasi, ni kiongozi wa kuzaliwa, ni mtu wakupenda kufanya kazi, si mtu wa kukata tama upesi na mara nyingi hupata mafanikio chanya kwasababu ya tabia hii, si mtu wa kutishwa kirahisi na daima husonga mbele, hapendi kuonewa, anapo ona jambo lina haribika hukemea mara moja hangoji mpaka mkutano ama kikao, ni mtu wa kujiamini, ni mshindani mzuri, ni mtu wa kujaribu, hakati tama mapema, ni mtu anayependa kutegemea maamuzi yake mwenyewe.
Udhaifu wa choleric:
Ni mtu mwenye hasira sana, ni mtu rough, ni mkali, ni mkorofi, hana shukrani, hawezi kuomba msamaha anapofanya kosa, hujiona yupo sahihi muda wote wakati sivyo,ni mbishi, si mtu wa kumaliza kazi, hajari wengine, hajari anacho ongea, ni mgumu kubadilika, anataka kuheshimiwa muda wote, ni mtu wa kuamrisha wengine.
3. TABIA YA MELANCHOLY
Sifa zake:
Ni mtu mkimya , hana maneno mengi, ni mchanganuzi, ni mtu wa vipawa vingi vya akili, ni mgunduzi (mfumbuzi wa vitu), ni mtu msafi na anaye jipenda, si mtu wa kusema ovyo au kutenda ovyo, hutumia akili kutatua mambo yanayo mkabili, ni mtu mwaminifu, si mtu wa kutoa siri ovyo, ana mapendo makamilifu kwa watu, ana uwezo sana wa kujizuia ktk kufanya mambo na siyo mwepesi wa kukata tamaa, ni mtu wa kujitolea, ni mbunifu na anajua mambo mengi sana, ni daktari mzuri sana.
Udhaifu wake:
Hana marafiki wengi, anachagua marafiki anao wapenda tu, anatunza hasira, ni mkimya sana, akiwa ana shida hazitoi kiurahisi hivyo ni rahisi kwake kuumizwa ndani kwa ndani, ni mtu anaye kosa amani pale anapofanya kosa Fulani kwa mwingine.
4. TABIA YA PHILEGMATIC
Sifa zake:
Ni mtu mpole na mtaratibu sana, sio mwepesi wa kuonyesha hasira, anaweza kukasirika lakini asionyeshe kama amekasirika, ni mtiifu wa asili, ni mtu mchekeshaji, anapendwa kuwekwa kuwa kiongozi ingawa yeye hapiganii uongozi, anaweza kujipanga, mwema, ana mapendo ya dhati, anamarafiki wengi.
Udhaifu wake:
Ni mwoga sana, si mwepesi wa kuamua jambo haraka, ni mzembe wa asili, ni msahaulifu, ni mvivu wa kazi, ana aibu sana, ni mtu wa kuonewa sana, ni mtu anayefanya kazi zake taratibu sana.
Mamb